Lusi akitaga mayai tunavunja


Mtoto mvulana wa miaka sita alikuwa na rafiki yake wa kike wa umri huohuo wanaishi nyumba zinaangaliana, siku hiyo akamwambia baba yake;
Mtoto: Baba mi nataka kuoa, baba yake kajichekea mwenyewe nae akamjibu
Baba: Ok unataka kumuoa nani mwanangu?
Mtoto: Namuoa Lusi, kwa vile baba alikuwa anamfahamu huyo Lusi akachekea tumboni tena,
Baba: Sasa mtaishi wapi?
Mtoto: Siku moja tutakuwa tunalala hapa kesho yake tunalala kwao
Baba:Usafiri je?
Mtoto: Mimi si nina baiskeli na yeye baba yake amemnunulia baiskeli
Baba: Sasa mkipata watoto itakuwaje
Mtoto: Watoto hatutaki, Lusi akitaga mayai tutakuwa tunayavunja
Baba: Okay

No comments:

Powered by Blogger.