HATUPIMI BANDO

WACHA TULALEEEEEE

WACHA TULALEEEEEE
WACHA TULALEEEEE

WADHAMINI

26 August 2012

HAWA NGURUWE HUWA WANANUNUA CHAKULA CHAO WENYEWE

Jamaa alikuwa anafuga nguruwe, siku moja akatembelewa na wanaharakati wa Haki za wanyama;
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesa wanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini... Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini....siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitakaNo comments: