Hii pantoni ya kwenda Kigamboni


Jamaa alimkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia, akamuuliza shida, yule mdada akasema maisha yamemshinda anaona heri ajiue. Jamaa akamwambia kuwa yeye ni baharia kwa hiyo akikubali atamuweka kwenye boksi kisha atamficha kwenye meli yake na wataweza kusafiri mpaka Ulaya wakifika huko atamuoa. Bibie akaona heri hilo akaingia kwenye boksi jamaa akambeba na kweli mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli, jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe analala huko kwenye hako kastoo,akimhakikishia mdada kuwa wanakaribia visiwa vya Komoro, na kisha hutoka na kuendelea na shughuli. Ilipita wiki ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo hicho, alipoulizwa akalazimika kueleza kila kitu, na kuwa anamuomba nahodha asimtupe baharini bali amlinde mpaka watakapofika Ulaya. Nahodha akamwambia mdada, 'Wala usipate taabu sikutupi popote, ila jamaa yako kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni, tukifika huko shuka'

No comments:

Powered by Blogger.